Wanne mbaroni kwa mauaji ya watu wenye vipara Msumbiji

MAPUTO-
POLISI katika jimbo la Zambezia nchini, wamewakamata watu wanne kwa madai ya kuhusika
na mauaji ya watu wenye vipara.
Wamesema
wanaendelea pia na uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo, huku wakifuatilia zaidi
kujua nani anachochea mauaji hayo.
Waganga wa
kienyeji wamekuwa wakidaiwa kusambaza habari zisizo na ukweli, kwamba vichwa
vya watu wenye vipara vina dhahabu ndani.
Pi, Polisi wamekuwa
wakichunguza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) ambao wanakatwa viungo
vyao vya mwili, na kutumika katika masuala ya imani za kishirikina.
Aidha,
wamesema washukiwa hao wa mauaji wanatoka katika nchi jirani.
BBC
No comments