Header Ads

Korea Kaskazini yarusha kombora kwenye bahari ya Japan



Korea Kaskazini imerusha kombora jingine la masafa marefu kutoka jimbo lake la magharibi kulingana na mamlaka ya Japan na Korea Kusini.
SEOUL- Korea Kaskazini imerusha kombora jingine la masafa marefu, kutoka jimbo lake la Magharibi kulingana na mamlaka za Japan na Korea Kusini.

Kombora hilo lilirushwa kutoka mji wa Bangyon, Kaskazini mwa mkoa wa Pyongyang kulingana na chombo cha habari cha Yonhap kikitaja duru za Jeshi la Korea Kusini.
Japan, imesema kuwa kombora hilo huenda lilianguka katika eneo la kiuchumi la bahari ya Japan. Korea Kaskazini imeongeza viwango vya majaribio vya makombora yake katika meizi ya hivi karibuni, hatua inayoendelea kuzua wasiwasi.
Kombora hilo la jana lilisafiri umbali wa kilomita 930 kwa dakika 40, kulingana na Korea Kusini na Japan. Hili ni kombora la 11 lililogunduliwa mwaka huu, lakini urefu wake umeongezeka kulingana na mwandishi wa BBC mjini Seoul, Stephens Evans.
Mara ya mwisho, Korea Kaskazini ilifanyia majaribio kombora lake mwezi uliopita. Ilirusha makombora yake katika wakati tofauti, yote yakielekezwa bahari ya Japan.
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Japan, Yoshihide Suga aliwaambia waandishi wa habari kwamba; “Uchokozi kama huu wa Korea Kaskazini hauwezi kukubalika. Tuliwasilisha malalamishi yetu na kushutumu hatua hiyo.”
Rais mpya wa Korea Kusini aliyechaguliwa hivi karibuni, Moon Jae-in ametaka kufanywa kwa mkutano wa dharura katika Baraza la Usalama la Taifa hilo.
Moon pia alikutana na Rais wa Marekani, Donald Trump wiki iliyopita, huku kiongozi huyo wa Marekani akiionya Pyongyang kwamba itapata jibu sahihi.
Kurushwa kwa kombora hilo kunajiri siku moja, baada Rais Trump kuzungumza kwa simu na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe na Rais wa China, Xi Jinping kuhusu Korea Kaskazini.
Viongozi hao walithibitisha jitihada zao za kuhakikisha kuwa hakuna utumizi wa nyuklia katika rais ya Korea.


No comments

Powered by Blogger.