‘Wanariadha wa kike wenye homoni za kiume wana uwezo mkubwa kuliko wenzao’

Caster Semenya. Mwanariadha huyu wa Afrika Kusini, ni mmoja kati ya wanariadha wanaodaiwa kuwa na homoni nyingi za kiume kiasi cha wengi kudhani kuwa ni mwanaume na si mwanamke.
LONDON- UTAFITI
mpya unasema kuwa wanawake wanaozaliwa na viwango vya juu vya homoni za kiume (Testosterone),
wana uwezo mkubwa wa utendaji ikilinganishwa na wenzao katika mashindano.
Hata hivyo,
watafiti hao wamebainisha kwamba ushirikiano kati ya viwango vya juu vya homoni
za testosterone na utendaji bora, haufai kuchukuliwa kama thibitisho.
Ripoti hiyo
iliyochapishwa katika jarida la matibabu katika michezo, inatokana na sampuli 100
za damu zilizochukuliwa kutoka kwa wanariadha katika kipindi cha miaka miwili.
Kuja kwa
ripoti hiyo ambayo imechapishwa wiki chache kabla ya Mahakama ya Usuluhishi
kuhusu masuala ya michezo, kutoa uamuzi wake wa mwisho kuhusu uamuzi wa
shirikisho la wanariadha duniani I.A.A.F kuwapiga marufuku wanariadha wa kike
walio na homoni nyingi za kiume.
Marufuku
hiyo iliyoanzishwa 2011, ilisitishwa na mahakama hiyo miaka miwili iliopita.
BBC
No comments