Header Ads

Auawa baada ya kujaribu kuiba helikopta ya polisi Marekani



screen-shot-2017-07-03-at-4-15-41-pm.png
HILLSBORO- MTU mmoja amepigwa risasi na kufa, baada ya kuruka uzio na kujaribu kuiba helikopta ya polisi mjini hapa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Koin TV mjini Portland, ilieleza kuwa mtu huyo aliyevalia kinyago cha kuficha sura, aliruka uzio na kuingia kwenye sehemu ya maegesho ya helikopta hizo akiwa na mwanafunzi wa urubani.
Mara baada ya kufanikiwa kuingia, aliwanyooshea silaha askari na kufyatua hewani risasi moja kabla ya kujaribu kutoroka kwa kuruka tena uzio na kuanza kukimbia.
Hata hivyo, mshukiwa huyo hakuweza kwenda mbali kwani alipigwa risasi na kufariki wakati akipatiwa huduma ya kwanza na askari walinzi wa eneo hilo.
CBS

No comments

Powered by Blogger.