Waliooa wanawake wengi washtakiwa Canada

Kiongozi wa kidini Canada, Winston Blackmore ambaye anadaiwa kuwa na watoto zaidi ya 145 na wanawake 24.
OTTAWA- VIONGOZI
wawili wa dini nchini, wamepatikana na hatia ya kuoa wake wengi.
Mahakama
iliambiwa kuwa, Winston Blackmore mwenye umri wa miaka 61 alioa wanawake 24, huku
mkwe wake James Oler akioa wanawake watano.
Wote
walipatikana na hatia ya shtaka moja la kuwaoa wanawake wengi na kila mmoja
anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela.

James Oler ambaye naye anadaiwa kuwa na wake watano.
Hukumu hiyo, imetajwa kuwa mtihani mkubwa kwa uhuru wa kidini nchini Canada. Blackmore na Oler wanatoka katika jamii moja ya dini, inayodaiwa kuwa na waumini 1,500 ambayo ilianzishwa mwaka 1946.
Hukumu hiyo, imetajwa kuwa mtihani mkubwa kwa uhuru wa kidini nchini Canada. Blackmore na Oler wanatoka katika jamii moja ya dini, inayodaiwa kuwa na waumini 1,500 ambayo ilianzishwa mwaka 1946.
Wote walikuwa
ni makasisi wa dhehebu lililojitenga, kutoka kanisa la Fundamentalist Church of
Jesus Christ of Latter-Day Saints (FLDS). Blackmore alifukuzwa kutoka FLDS
mwaka 2002 na mahala pake pakachukuliwa na Oler.
Matawi ya
dhehebu hilo yako nchini Marekani, ambako kuna wanachama karibu 10,000. Kuoa
wanawake wengi ni haramu chini ya sheria za Canada na Polisi walianza
kuchunguza dhehebu hilo kuanzia miaka ya 1990.
BBC.
No comments