Marekani; Korea Kaskazini iko mbioni kujaribu kombora lingine
SEOUL- KWA mujibu
wa habari za kiintelijensia kutoka Idara ya Mambo ya Ndani ya Marekani, Korea
Kaskazini kwa sasa inajiandaa kufanya majaribio ya kombora lingine ambalo bado halijajulikana.
Maofisa wa
idara hiyo, wanadai kuwa wamebaini kuwasili kwa magari yanayobeba vifaa vya
kujaribia makombora, katika eneo la Kusong lililo Kaskazini mwa taifa hilo
tangu Ijumaa ya wiki iliyopita.
Aidha,
maofisa hao wanadai kuwa vifaa hivyo vinapoonekana kwenye eneo hilo basi
jaribio lazima lifanyike ndani ya siku sita. Pia, inadaiwa kuwa huenda ni
maandalizi kwa ajili ya kujaribu kombora siku ya Julai 27, ambayo ni
maadhimisho ya Makubaliano Matukufu yaliyomaliza vita baina ya Korea Kaskazini
na Kusini.
Jumatano ya
wiki iliyopita, Shirika la Habari la CNN liliripoti kuwa wanaintelijensia wa
Marekani wamebaini uwepo wa maandalizi ya jaribio la kombora lingine la aidha
kutoka bara moja hadi jingine (ICBM) au kombora la masafa mafupi.
Maofisa wawili
walisema kuwa, satalaiti ya Marekani ilionesha picha hizo na rada kwenye
satalaiti hiyo ilionesha uwezekano wa taifa hilo kufanya jaribio hilo.
Eneo la
Kusong limekuwa maarufu kwa majaribio ya makombora, ambapo Mei mwaka huu
walifanya jaribio la kombora la masafa mafupi la KN-17 ambalo limesafiri kwa
maili 500 kabla ya kutua Mashariki mwa bahari ya Japan.
CNN
No comments