Mezani Asubuhi; Conte amwagiwa noti Chelsea # Renato Sanches ruksa Man Utd # Sanchez kununua mkataba wake Arsenal
LONDON- KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte amepewa fungu
jipya la pauni milioni 150 (sh bilioni 435) kwa ajili ya kutumia kwenye zoezi
la usajili msimu huu.
Katika orodha yake kuna majina ya Virgil van Dijk wa Southampton, Alex
Sandro wa Juventus, Antonio Candreva wa Inter Milan, Tom Davies wa Everton na
Fernando Llorente wa Swansea City. Daily Mirror.

Carlo Ancelotti ameiambia Manchester United kuwa, wanaweza kumsajili
kiungo wa Bayern Munich na Ureno, Renato Sanches (19) lakini wasahau kuhusu
mpango wao wa kumsajili Arturo Vidal (30) kwani hauzwi. Independent.

Winga wa Arsenal, Alexis Sanchez (28), yuko tayari kulipa fedha kwa ajili
ya kununua mkataba wake ili aruhusiwe kujiunga na Manchester City. Pia, raia
huyo wa Chile anasakwa na Juventus ya Italia. Independent.
PSG imesema
itamtoa kiungo wao, Marco Verratti (24) na pauni milioni 90 (sh bilioni 261),
kwa Barcelona ikiwa ni sehemu ya usajili wa mshambualiji raia wa Brazil, Neymar
(25). Diario Gol.
Roma ya Italia, imeweka mezani dau la pauni milioni 30 (sh bilioni 87)
kwa ajili ya kumsajili winga wa Leicester City, Riyad Mahrez (26) lakini klabu
hiyo maarufu kama Mbweha, wanataka pauni milioni 50 (sh bilioni 145). Daily
Mail.

Everton inaamini kuwa dau lao la pauni milioni 45 (sh bilioni 130.5),
litakubaliwa na Swansea, kama ada ya uhamisho wa kiungo wao, Gylfi Sigurdsson
(27) na kukamilisha usajili huo ifikapo Alhamis wiki hii. Daily Mail.
Klabu ya Galatasaray inahusishwa na mpango wa kumnunua kiungo wa Arsenal
na Misri, Mohamed Elneny (25). Fotospor.
Marseille inafanya
mazungumzo na klabu ya Celtic ya Scotland, kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji
wao kinda, Moussa Dembele (20) kwa dau la pauni milioni 20 (sh bilioni 58). Daily Express.
Borussia Dortmund
wanataka kumsajili winga wa Man City, Jadon Sancho (17), ambaye hatima yake iko
shakani klabuni hapo kutokana na kutosainishwa mkataba. ESPN.
Mshambuliaji
wa Arsenal, Lucas Perez anataka kuondoka klabuni hapo kutokana na kuhisi kuwa
hatendewi haki. Hiyo inakuja baada ya klabu hiyo kumsajili Alexandre Lacazette
na kumpa jezi namba 9 aliyokuwa akiitumia yeye (Perez). Daily Telegraph.
No comments