Header Ads

Urusi yajibu vikwazo vya Marekani



https://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/14BA5/production/_97110948_gettyimages-630672230.jpg

MOSCOW- WAKATI Bunge la Senate la Marekani kuidhinisha muswada wa vikwazo vipya, Urusi imelitaka taifa hilo kupunguza watumishi wake wa ubalozi mjini hapa hadi kufikia 455.
Aidha, Urusi imesema imetwaa baadhi ya miundombinu inayotumika kwenye shughuli za kibalozi kama Marekani ilivyofanya mwaka jana. Mwaka jana, Marekani ilitaifisha majengo mawili ya Urusi, yaliyokuwa yakitumika katika shughuli za kibalozi nchini humo.
Hata hivyo, uamuzi wa Urusi unatarajiwa kutozuia vikwazo vingine ambavyo vimewekwa na Marekani kwa madai kuwa Urusi kulitwaa kinguvu jimbo la Crimea la Ukraine mwaka 2014.
Pia, kumekuwa na uchunguzi unaoendelea iwapo Urusi imeingilia uchaguzi wa taifa hilo uliofanyika mwaka jana.
BBC.

No comments

Powered by Blogger.