Mezani Jioni; Barca kutoa £81m na Rakitic Liverpool # Neymar azichapa mazoezini # Sanchez kuchelewa mazoezi Arsenal
BARCELONA-
BARCELONA wamesema wapo tayari kutoa pauni milioni 81 (sh bilioni 234.9),
pamoja na kiungo wao, Ivan Rakitic ikiwa ni sehemu ya dili la uhamisho wa
Philippe Coutinho kutoka Liverpool kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa La Liga.
Sakata la usajili wa
mshambuliaji wa Barcelona, Neymar, limezidi kuchukua sura mpya, baada ya
mchezaji huyo kuahirisha safari ya kwenda China kukutana na mashabiki wake. Pia,
Neymar alisababisha mazoezi ya timu hiyo kuvunjika kutokana na kugombana na
mchezaji mwenzake.
Wakala wa Gareth Bale,
Jonathan Barnett amepuuza ripoti zinazodai kuwa mteja wake ataondoka Real
Madrid ni upuuzi mtupu. Barnett amedai Bale hawezi kuondoka Real Madrid. Hata hivyo,
kocha wa Madrid, Zinedine Zidane alisema lolote linaweza kutokea msimu huu wa
usajili.
Alexis Sanchez ambaye
alitarajiwa kurejea mazoezini Jumapili ijayo, sasa anaweza kuchelewa zaidi,
baada ya kupost picha yenye maelezo kwamba anaumwa. Kocha wa Arsenal, Arsene
Wenger alitarajia kuwa Sanchez atajiunga na wenzake mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa Bayern
Munich, Karl-Heinz Rummenigge amesema kocha wa Chelsea, Antonio Conte ameulizia
kuhusu upatikanaji wa kiungo Renato Sanches. Hata hivyo, Rummenigge ameeleza
kuna timu 10 zinazomhitaji mchezaji huyo.
Kocha wa Manchester
City, Pep Guardiola amesema anatamani kuongeza mkataba na timu hiyo lakini
hatima yake klabuni hapo itaamuliwa na idadi ya vikombe atakavyotwaa msimu ujao.
Mchezaji mpya wa West
Ham, Javier Hernandez ‘Chicharito’ amesema alilazimika kuzipiga chini ofa
kutoka Hispania na Italia, ili aweze kurudi kwenye ligi bora ya England maarufu
‘EPL’.
Kocha wa Newcastle
United, Rafael Benitez amesema anajisikia vema baada ya kufanikiwa kumsajili
kinda kutoka Borussia Dortmund, Mikel Merino kwani ni mmoja kati ya viungo bora
vijana.
Sky Sports.
No comments