Uruguay yaweka rekodi kwa kuhalalisha rasmi biashara ya bangi
MONTEVIDEO- URUGUAY
imeingia kwenye vitabu vya kumbukumbu za dunia, kwa kuwa nchi kwanza
kuhalalisha mauzo ya bangi kwa minajili ya kujiburudisha.
Maduka 16 ya
kuuza mmea huo yalianza rasmi kuuza bangi jana. Karibu watu 5,000 wamejiandikisha
Serikalini, ili waweze kununua bangi kwa njia halali.
Hata hivyo,
watumiaji wa mmea huo maarufu zaidi duniani, watalazimika kujibana kwani
wataruhusiwa kununua hadi gramu 10 kwa wiki na manunuzi yao yasizidi gramu 40
kwa mwezi.
Hatua hii
inakuja miaka minne, baada ya sheria iliyohalalisha biashara ya bangi kupitishwa.
Wale wanaounga mkono wanasema itasaidia kukomesha biashara haramu ya bangi na
kuwatupa nje wauza madawa ya kulevya.
Wafanyabiashara
wanaweza kuchagua kutoka aina mbili ya bangi kati ya Alpha 1 na Beta 1. Bei ya
gramu tano za bangi itauzwa dola 6.50 (sh 14,300).
Bangi
inayouzwa kwenye maduka ya madawa, hutoka kwenye mashamba yanayosimiwa na Serikali.
Pia, sheria
hiyo huwaruhusu watu kupanda bangi yao nyumbani au kujiunga na vilabu
vinavyofanya kilimo cha mmea huo.
No comments