Mali za rais wa Brazil kushikiliwa
BRASILIA- Jaji
wa Mahakama Kuu nchini, Sergio Moro ameagiza mali za Rais wa zamani wa Brazil, Luiz
Inacio Lula da Silva kushikiliwa, baada ya kupatikana na hatia ya rushwa.
Jaji Moro
amesema kiasi cha fedha zenye thamani ya dola za Marekani 200,000 (sh milioni
440) zimegunduliwa katika akaunti ya kiongozi huyo wa zamani.
Majengo
matatu ya ghorofa, kipande cha ardhi na magari mawili pia yanashikiliwa
kufuatia amri hiyo iliyotolewa.
Lula ambaye
alipata umaarufu kwa uongozi wake nchini, ataendelea kutumia mali zake, lakini
iwapo rufaa aliyokata kupinga kifungo cha miaka tisa gerezani alichohukumiwa,
itashindwa, mali hizo zitakamatwa.
Mwenyewe
amekuwa akidai kuwa mashtaka dhidi yake yamehamasishwa kisiasa.
BBC
No comments