Mtoto aliyepandikizwa mikono aanza kucheza mpira wa magongo
PHILADELPHIA-
KIJANA wa kiume nchini, Zion Harvey ameweka historia kwa kuwa mtoto wa kwanza
kupandikizwa mikono na kuweza kucheza ipasavyo mpira wa magongo (Baseball).
Ni miaka
miwili tangu Zion ambaye sasa ana umri wa miaka 10, apandikizwe mikono mipya,
na madaktari wake wanasema wamefurahishwa na namna anavyoendelea.
Zion kwa
sasa anaweza kuandika, kujilisha na pia kujivisha nguo. Licha ya mikono yake
kutoka kwa mtu mwingine, ubongo wake umeikubali kama yake, kwa mujibu wa uchunguzi
uliofanywa.
Zion
alizaliwa akiwa na mikono yote miwili, lakini wakati alipofikisha umri wa miaka
miwili, madaktari walilazimika kuikata.
“Wakati nilipokuwa
na umri wa miaka miwili, mikono yangu ilikatwa kwa sababu nilikuwa mgonjwa,” anasema
Zion.
Zion alikuwa
na ugonjwa ujulikanao kama Sepsis, ambao ni hatari kwa maisha. Madaktari
walikata mikono yake kwa sababu ilikuwa inakufa. Pia figo zake zilipata
matatizo.
Akiwa na
umri wa miaka minne, Zion aliwekewa figo kutoka kwa mama yake. Upasuaji wa
kumuwekea Zion mikono, uliofanywa Juni 2015, ulikuwa hatua kubwa.
Kando na ule
uliofanywa mwaka 1998, upasuaji wake Zion alifanyiwa mtu mwenye umri mdogo
zaidi.
Kundi la
watu 40 wakiwemo madaktari wa upasuaji 10, walimfanyia Zion upasuaji usiku wote
hadi asubuhi kumpandikiza mikono yake mipya.
Changamoto
kubwa waliyokumbana nayo madaktari wakati wa upasuaji wa Zion, ilikuwa ni
kuunganisha mishipa midogo ya damu ambayo ingesaidia mikono yake kubaki kuwa
hai.
BBC.
No comments