Header Ads

Ukuaji wa uchumi China wafikia asilimia 6.9



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiyt_M1OGhqq0O1VaDw5Mjgmj9NHkAGtCXAtmwD3iwIhO7xSx7HQCdtdYkBnJ-9YjOaX6pSXrwq79EDSXUZQd3e7CNpK9eUq3SQ1PuGBDDMR7NDcOsWUfbmzVN7mL_KCM-N0POYy0S5kUYf/s1600/china.jpg

HONG KONG- TAKWIMU za Uchumi, zinaonesha kuwa uchumi wa China ulikua kwa asilimia 6.9 kati ya Aprili na Juni na kuvuka matarajio ya wengi ambao awali hawakuweka kadiro hilo.
Ukuaji huo ambao ni mkubwa ukilinganishwa na miezi mitatu iliyopita, ulikuwa sawa na robo ya kwanza ya mwaka 2017.
Wachanganuzi wengi, walitarajia kuwa uchumi wa China huenda ukapunguza kasi ya ukuaji wake. Lakini, takwimu za hivi punde ziko juu kuliko matarajio ya ukuaji wa asilimia 6.5.
Licha ya jitihada za kupunguza uwekezaji katika nyumba, uwekezaji katika sekta za ujenzi ulikua kwa asilimia 8.5 katika robo ya kwanza ya mwaka, ambayo ni juu kutoka kipindi kama hicho mwaka 2016.
Wadadisi wanatabiri kuwa sheria ngumu za ukopeshaji haziwezi kuathiri uwekezaji kama wengi walivyotarajia.
BBC

No comments

Powered by Blogger.