Header Ads

Sitashiriki mdahalo wa wagombea wenza kwani sijaalikwa- Ruto



President Uhuru Kenyatta and Deputy President William Ruto during a political rally in Malindi on Sunday, July 16, 2017. /DPPS

NAIROBI- NAIBU Rais nchini, William Ruto, amesema hatohudhuria mdahalo wa wagombea wenza ambao unafanyika leo kwa kuwa hajawahi elezwa kuhusu jambo hilo wala kualikwa.
Mdahalo huo baina ya Ruto, mpinzani wake ambaye ni mgombea mwenza kutoka Muungano wa NASA, Kalonzo Musyoka na wengine kutoka vyama vingine, ulitarajiwa ufanyike kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Katoliki cha Afrika Mashariki jijini hapa.
“Nimeshangazwa sana kutokana na kuwa, hakuna hata mtu mmoja aliyenishirikisha kwenye jambo hilo (mdahalo). Kiutaratibu, ilihitajika niambiwe kuhusu tarehe, muda, taratibu za ushiriki na sheria zake na mambo mengineyo,” alisema Ruto.
Kiongozi huyo alisema kuwa, si uungwana kusikia kuwa kuna mdahalo huo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
The Star.

No comments

Powered by Blogger.