Ujio wa Lacazzette utamshawishi Sanchez kubaki Arsenal

LONDON- UJIO wa mshambuliaji wa kati, Alexandre Lacazzette ambaye jana
alikamilisha vipimo vya afya katika klabu ya Arsenal, huenda ukambakiza klabuni
hapo Alexis Sanchez.
Kwa mujibu wa mmoja wa wachambuzi nguli wa soka Uingereza, Nigel
Winterburn, ujio wa Lacazzette unatarajiwa kuhuisha ndoto za Arsene Wenger
kumbakiza Sanchez klabuni hapo ili asaidiane kazi na mshambuliaji huyo kutoka
Ufaransa.
“Ninafikiri iko wazi kwa mashabiki wa Arsenal na hata kwake Wenger kuwa,
sehemu ya muhimu zaidi ya kuiongezea nguvu ni safu ya mbele ya timu hiyo,”
“Hivyo natumaini kuwa Giroud atabaki, kwani nafikiri bado ni mtu
anayehitajika kwenye timu. Arsenal wanafahamu kuwa, wanahitaji wachezaji bora
ili kuwasaidia kupambana kwa ajili ya ubingwa”
“Na kwa namna yoyote ile, Sanchez atashawishika kubaki na atakuwa
akicheza winga ya kushoto au kulia ama nyuma ya mshambuliaji. Kwa pamoja
wataing’arisha Arsenal, hivyo hawawezi kwa namna yoyote kumnunua Lacazzette kwa
pauni milioni 52 na kumwachia Sanchez aondoke ndani ya wiki mbili zijazo,”
alisema Winterburn.
Sky Sports
No comments