Header Ads

Uingereza yadai Saudi Arabia inafadhili wenye misimamo mikali ya kidini



Msikiti Saudia
LONDON- RIPOTI Mpya na taasisi ya Henri Jackson Society, imeeleza kuwa Saudi Arabia ndiyo mfadhili mkuu wa watu wenye misimamo mikali ya kidini nchini.

Ripoti hiyo imesema kuwa, kuna ushirikiano wa wazi kati ya mashirika ya Kiislamu yanayotoa ufadhili kwa wahubiri wenye chuki na makundi ya kijihad yanayokuza ghasia.
Idara ya Mmambo ya Nje ilitaka kuchunguzwa kwa jukumu la Saudi Arabia na mataifa mengine ya Ghuba. Ubalozi wa Saudia nchini, umesema kuwa madai hayo ni ya ‘uongo’.
Mawaziri wanakabiliwa na shinikizo ya kuchapisha ripoti ya makundi ya Kiislamu yaliyoko nchini.
Ripoti hiyo ya Idara ya Mambo ya Ndani, kuhusu uwepo wa makundi ya kijihad iliyoanzishwa na aliyekuwa Waziri Mkuu, David Cameron mwaka 2015, bado haijakamilika na kuna ripoti za iwapo itachapishwa au la.
Wakosoaji wanasema kuwa huenda ikawa vigumu kwa Serikali kuisoma, kutokana na ushirikiano wa karibu wa kidiplomasia, usalama, kiuchumi na mataifa ya Ghuba hususan Saudi Arabia.
Ripoti hiyo ya leo, inasema kuwa mataifa kadhaa ya Ghuba ikiwemo Iran yanatoa ufadhili wa kifedha kwa misikiti na taasisi za elimu ya Kiislamu ambazo zimekuwa zikiwakuza wahubiri wa chuki, suala linalosababisha kuenea kwa Itikadi kali.
Katika kilele cha orodha hiyo, ripoti hiyo inasema ni Saudia. Inadai kwamba, watu binafsi na wakfu wamehusishwa kueneza itikadi za Wahabby ikinukuu mifano kadhaa.
Katika visa vingine vichache, ripoti hiyo inadai taasisi nchini zinazopokea ufadhili wa Uingereza zinatekeleza operesheni zake moja kwa moja kutoka Saudia, ijapokuwa fedha hizo huonekana kununua ushawishi wa wafadhili wa kigeni.
Katika taarifa yake ubalozi wa Saudia mjini hapa, unasema kuwa tuhuma zozote kwamba ufalme huo unafadhili watu wenye itikadi kali, hazina msingi na wala ushahidi wowote.
Imesema kuwa taifa hilo limeshambuliwa na Al-Qaeda na wapiganaji wa Islamic State.
Imeongezea kwamba: “Hatuungi mkono na hatuwezi kuunga mkono vitendo vya makundi yenye itikadi kali, na hatutapumzika hadi makundi hayo yaliokosa mwelekeo na mashirika yao yaangamnizwe.”
BBC

No comments

Powered by Blogger.