Boko Haram waua na kuteka wanawake Niger
NIAMEY-
KUNDI la wanamgambo wa
Kiislamu la Boko Haram, limedaiwa kuua watu tisa na kujeruhi watu kadhaa na
kuteka wengine wanaokadiriwa kufikia 40 katika kijiji cha NGalewa kilichopo
Mashariki mwa mji wa Diffa nchini.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Adam Babakarna, alisema kuwa wanamgambo
hao waliwasili kijijini hapo Jumapili jioni kwa kutumia ngamia na farasi na
kisha kuanza kutekeleza unyama huo.
Babakarna alisema kuwa wengi wao wa waliochukuliwa mateka na wanamgambo
hao, ni wanawake na watoto na kutishia kuwashikilia hadi hapo wapiganaji wenzao
watakapoachiliwa na Serikali.
“Wapiganaji wanaoaminiwa kuwa ni Boko Haram, wameua watu tisa kwa kuwachinja
na kisha kuondoka na wanawake wapatao 37. Vyombo vya ulinzi tayari vinafuatilia
tukio hilo kwa ukaribu,” alisema Gavana wa Diffa, Laouali Mahamane Dan Dano
wakati alipokuwa akizungumza na televisheni ya Serikali.
Aidha, Dan Dano alisema kuwa anatumai kuwa vyombo hivyo vitabaini maficho
ya wanamgambo hao na kisha kuwakomboa wanawake hao.
CBS
News
No comments