China kufanya majaribio ya 5G mwaka huu

BEIJING-
KAMPUNI kubwa za simu nchini, zinatarajiwa kuongoza mpango wa usimikaji na
uwezeshaji wa teknolojia ya kasi zaidi ya 5G kwa majaribio, kwenye miji kadhaa
katika kipindi cha nusu ya pili ya mwaka huu.
Miji hiyo inayotarajiwa
kuwepo kwenye orodha hiyo ya kupata huduma hiyo ya intanet yenye kasi zaidi ni,
Beijing, Shanghai, Chongquing, Guangzhou, Nanjing, Suzhou na Ningbo.
Kampuni hizo
zinazotarajiwa kusimika na kusimamia matumizi ya 5G ni, China Mobile, China
Unicom na China Telecom.
No comments