Trump ajutia kumteua Sessions kuwa Mwanasheria Mkuu
NEW YORK- Rais
Donald Trump amesema kuwa asingemteua Jeff Sessions kuwa Mwanasheria Mkuu, kama
angejua kuwa angejiondoa kutoka kuongoza uchunguzi kuhusu Urusi.
Trump ameliambia
gazeti la New York Times kuwa, hatua ya Sessions haijawa nzuri kwa urais. Sessions
alijiondoa baada ya kukiri kuwa alikutana na Balozi wa Urusi.
Alisema kuwa
hawezi kujiuzulu, na ataendelea kuongoza idara ya sheria vyema. Sessions
alikuwa mmoja wa wale waliomuunga mkono zaidi Trump.
Licha ya
gavana huyo wa zamani wa Alabama kuwa na jukumu la kutekeleza ajenda ya Rais
kama mwanasheria mkuu, Trump mwenyewe anamlaumu kwa kuruhusu kuwepo kwa
uchunguzi huru ambao umehujumu Urais.
Aliyekuwa Mkurugenzi
wa FBI, James Comey, ambaye mwenyewe alilengwa na Trump, alifichua kuwa kundi
la kampeni ya Trump lilikuwa chini ya uchunguzi.
BBC
No comments