Asubuhi Njema; Barcelona wamfuata Coutinho # United wamgeukia Aurier # Spurs wamtaka Mahrez
LIVERPOOL- Barcelona wameweka mezani mwa Liverpool dau
la pauni milioni 72 (sh bilioni 208.8), kwa ajili ya kumnunua kiungo mahiri,
Philippe Coutinho (25). Hata hivyo, Liverpool wanasemekana kuwa watakataa dili
hilo. Mail.
Manchester United wameelekeza pauni milioni 25 (sh bilioni 72.5) kwa PSG,
ili kumsajili beki Serge Aurier (24) wakati wakihangaika kumsajili kiungo wa
Monaco, Fabinho (23). Kocha wa PSG, Unai Emery, amethibitisha kuwa beki wake
raia wa Ivory Coast, anataka kuondoka klabuni hapo msimu huu. Independent.
Arsenal wamezidi kupata matumaini makubwa, kwamba kiungo wao mahiri,
Mesut Ozil (28) atasaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya
London. Sun.
Tottenham Hotspurs imeomba iwe inapewa taarifa kuhusu hatima ya Riyad
Mahrez (26), klabuni Leicester City lakini ikiiambia klabu hiyo ipunguze dau
lao la pauni milioni 50 (sh bilioni 145) ili waweze kumsajili. Standard.
Monaco imepiga chini dau la pauni milioni 44.5 (sh bilioni 129), kutoka
Manchester City kwa ajili ya beki wao wa kati, Benjamin Mendy (23). Mabingwa hao
wa Ufaransa wanadai Mendy anauzwa kwa pauni milioni 54 (sh bilioni 156.6). Mail.
Manchester United bado haijafikia makubaliano na Inter Milan, kuhusu
thamani halisi ya winga wa timu hiyo na Croatia, Ivan Perisic (28). Inter wanadai
kumuuza kwa pauni milioni 48 (sh bilioni 139.2), lakini United hawataki kutoa
kiasi hicho. Mail.
Arsenal na Tottenham wameingia kwenye mbio za kumnyatia kinda wa
Manchester City, Jadon Sancho. Independent.
Mshambuliaji mpya wa klabu ya West Ham, Marko Arnautovic (28),
anatarajiwa kuwa mchezaji anayelipwa zaidi klabuni hapo, endapo atafuzu vipimo
vya afya leo. Express.
Crystal Palace wanatarajiwa kuwasilisha ofa ya pili mezani mwa Arsenal,
kwa ajili ya kumsajili beki wao, Calum Chambers (22), baada ya ofa ya kwanza
yenye thamani ya pauni milioni 16 (sh bilioni 46.4) kukataliwa. ESPN.
No comments