Mtoto wa Simba Cecil wa Zimbabwe auawa
Cecil enzi za uhai wake kabla ya kuuawa mwaka 2015.
HARARE- MIAKA
miwili baada ya simba dume aitwaye Cecil, kuuwawa na mwindaji nchini na kuzua
shutuma kimataifa, mwanawe naye ameuwawa.
Xanda, simba
mtoto mwenye umri wa miaka sita, alipigwa risasi na mwindaji na anaripotiwa kufia
nje ya mbuga ya Hwange iliyopo Kaskazini mwa nchi.
Katika juhudi
za kuzuia ujangili, Serikali kwa kushirikiana na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha
Oxford walilazimika kumuwekea Xanda kifaa maalum cha kumfuatilia.
Mwandishi wa
BBC Harare, anasema kuwa akiwa na umri wa miaka sita, Xanda alikuwa amefikia
umri wa kuweza kulengwa na wawindaji.
Wawindaji hao,
wengi wao kutoka Marekani, Uingereza na Afrika Kusini, hulipa maelfu ya fedha kwa
ajili ya kuruhusiwa kuwinda, na fedha hizo hutumiwa kugharimia watu ambao
huwalinda wanyamapori.
Haijulikani
ni nani alikuwa amelipa fedha ili kumuua Xanda.
No comments