Tottenham haiuzwi na wala haina mpango wa kuuzwa

LONDON- UONGOZI wa klabu ya soka ya Tottenham Hotspurs
iliyopo London Kaskazini, umesema kwamba timu hiyo haiuzwi na hakuna mpango
wowote wa kuiuza.
Taarifa iliyotolewa
na Bodi ya timu hiyo, ilieleza kuwa klabu hiyo haiuzwi na wala hakuna mpango wa
kuiuza; “Bodi haipo kwenye mazungumzo ya aina yoyote yale yenye lengo la kuiuza
klabu.”
“Bodi
inaamini kuwa (makubaliano ya ufadhili wa uwanja huo), ilikuwa ni suluhisho
tosha kwa matakwa ya mashabiki, waajiriwa na washika dau na kwa maendeleo ya
klabu hii.”
Hayo yanajiri
baada ya vyombo vya habari kudai kuwa, kampuni ya Iconiq Capital iko tayari
kuinunua klabu hiyo ambayo msimu uliopita ilishika nafasi ya pili Ligi Kuu ya
Uingereza nyuma ya mabingwa, Chelsea.
Habari hizo
zinakuja wakati Tot wakiuhama uwanja wao wa White Hart Lane na kuhamia Wembley
ili kupisha ujenzi. Tayari benki tatu za Bank of America Merrill Lynch
International Ltd, Goldman Sachs Bank USA na HSBC Bank zimekubali kufadhili
ujenzi huo.
BBC Sport
No comments