Mdee afikishwa mahakamani na kuachiwa kwa dhamana
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (aliyevaa koti jeupe) akisalimiana na Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kufikishwa mahakamani hapo leo.
DAR ES SALAAM- MBUNGE wa
Kawe, Halima Mdee, hatimaye amefikishwa katika Mahakama ya Hkimu Mkazi Kisutu
Dar es Salaam na kuachiwa kwa dhamana.
Awali, Mdee alikuwa akishikiliwa katika kituo cha polisi cha Oysterbay kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi kabla ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati. Hata baada ya Masaa 48 kuisha, hakuachiwa huru kwani aliendelea kushikiliwa.
Hata hivyo, Mdee ameachiwa kwa dhamana ya Milioni 10 na wadhamini wawili. Ushahidi haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Agosti 7, 2017.
No comments