Jinamizi la moto lazidi kuiandama London
LONDON-
JINAMIZI la moto limezidi kuiandama Uingereza, baada ya moto mkubwa kuzuka
ghafla katika soko la Camden Lock Market na kusababisha hasara kubwa.
Zaidi ya
watumishi 70 na injini 10 za kuzimia moto kutoka katika Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji, zilitumika kupambana na moto huo mkubwa ambao ulizuka majira ua 2:50
alfajiri (kwa saa za Uingereza).
Licha ya
moto huo kuwa mkubwa, Kikosi cha Zimamoto cha London kimeeleza kuwa hakukuwa na
mtu yeyote aliyejeruhiwa.
Moto huo
ambao bado chanzo chake hakijajulikana, unakuwa wa pili kuteketeza soko hilo
baada ya ule wa kwanza uliotokea mwaka 2008 na kusababisha hasara.
Soko hilo
linadaiwa kutembelewa na watu zaidi ya milioni 28 kila mwaka, wengi wao wakiwa
wanaenda kufanya manunuzi huku wengine wakienda kufanya utalii sokoni hapo.
ABC News
No comments