Tetesi za usajili leo Julai 3, 2017

LONDON- MANCHESTER
United na Paris St-Germain wako tayari kutoa £174m kumfungua mshambuliaji wa
Barcelona Neymar kutoka kwa mkataba wake katika klabu hiyo iwapo mchezaji huyo
ataamua kuihama klabu hiyo ya Uhispania (Don Balon kupitia Daily Star).
Arsenal
wanakaribia kutangaza usajili wa winga kutoka Algeria, Riyad Mahrez, 26 ambaye
anaichezea Leicester City (Calciomercato).
Arsenal
huenda wakakamilisha usajili wa Alexandre Lacazette, 26, katika saa 48 zijazo
kwa mujibu wa rais wa Lyon Jena-Michel Auylas (Le Progress).
Paris Saint
Germain wamemuulizia kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, huku Liverpool
wakisema mchezaji huyo kutoka Brazil ana thamani ya pauni milioni 87 (Daily
Mirror).

Chelsea wana
matumaini wataweza kufanikisha mpango wa kumsajili beki wa kushoto kutoka
Brazil, Alex Sandro, (pichani), huku mazungumzo na Juventus yakitarajiwa kufanyika
Jumatatu (Daily Telegraph).
Antonio
Conte anakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City katika kutaka kumsajili
beki wa kati wa Roma Antonio Rudiger, 24. Barcelona pia wanataka kumsajili
Leonardo Bonucci, 30, ambaye Chelsea wanamtaka, na Juventus wamempa mkataba
mpya Sandro ili kumsawishi asiondoke (Daily Mirror).
Jurgen Klopp
ameiambia Liverpool kuongeza bidii katika kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby
Keita, 22, ambaye atakuwa na mazungumzo na klabu yake kuhusu mustakbali wake
nchini Ujerumani (Times).
Nahodha wa
zamani wa England na Chelsea John Terry, 36, anatazamiwa kuthibitishwa kuwa
mchezaji wa Aston Villa siku ya Jumatatu (Daily Telegraph).
Kocha mkuu
wa Monaco Leonardo Jardim ana matumaini kuwa Kylian Mbappe, 18, hataondoka,
lakini amekiri kuwa wachezaji wengi huenda wakaondoka msimu huu (RMC).
Tottenham
wamepanda dau kwa mara ya pili la pauni milioni 27 kumtaka kiungo wa Sporting
Lisbon Adrien Silva, 28, (A Bola).
Chelsea
wamemuulizia beki wa Real Madrid Danilo, 25 (Marca).

Beki wa
Paris St-Germain anayenyatiwa na Manchester City, Marquinhos, 23, amesaini
mkataba mpya wa mude mrefu kubakia Ufaransa (Independent).
Newcastle
wanafikiria kumchukua beki wa Arsenal Kieran Gibbs (Daily Mirror).
Paris Saint-Germain
wamemuulizia kiungo mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, huku Barcelona
pia wakimnyatia mchezaji jhuyo kutoka Brazil (Daily Mirror).
No comments