Malinzi na mwenzake warudishwa rumande kwa kukosa dhamana

DAR ES SALAAM- RAIS wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, Katibu Mkuu wa TFF, Celestine
Mwesigwa na Mhasibu wa TFF, N Mwanga kwa pamoja wamekosa dhamana na kurudishwa
rumande hadi pale kesi yao itakapotajwa tena Julai 17 mwaka huu.
Hayo yamejiri leo
katika Mahakama ya Kisutu jijini hapa, baada ya kesi yao kutajwa baada ya hapo
awali kunyimwa dhamana kutokana na kesi 28 ambazo 25 zinamkabili Malinzi peke
yake na 3 zinawakabili wote kwa pamoja.
Kesi yao itatajwa tena
Julai 17, mwaka huu.
No comments