Tetesi za usajili leo; Everton yamwinda Rooney, #Mourinho akereka Man United, #Arsenal ikiwawinda ‘pacha’ wa Sporting Lisbon ya Ureno
LONDON- KWA
mujibu wa ripoti maalum ya wavuti ya michezo ya Talksport, imebainika kuwa
klabu ya Everton inafanya kila liwezekanalo ili kumsajili mshambuliaji wa timu
ya Manchester United na Uingereza, Wayne Rooney, msimu huu.
Hatua hiyo
ni sawa na kumrudisha mshambuliaji huyo nyumbani, kwani maisha ya mpira ya
Rooney yalianzia hapo Goodson Park kabla ya kutimkia Man United mwaka 2004.



Kocha wa Manchester
United, Jose Mourinho (pichani) ameonekana kukerwa na kile alichokiita kuwa mwendo wa
pole wa klabu hiyo kwenye suala la usajili wa wachezaji msimu ujao.
Licha ya
kuwa tayari ana beki Victor Lindelof kutoka Benfica, bado Mreno huyo
haridhishwi na spidi ndogo ya klabu hiyo kwenye usajili kwani wanachelewa
kukamilisha dili la mshambuliaji Alvaro Morata kutoka Real Madrid na kiungo wa
Chelsea, Nemanja Matic.
“Mtendaji
Mkuu wa Man United, Ed Woodward mwishoni mwa mwezi uliopita, alisafiri kwenda
New Zealand kuangalia mchezo wa rugby kati ya New Zealand na Uingereza. Kitendo
hicho kimemstaajabisha Mourinho na wenzake klabuni hapo,” limeandika gazeti la
The Guardian.

Gazeti la
The Telegraph limeandika kwamba, klabu ya West Ham United inahitaji huduma za
mchezaji wa zamani wa Manchester United, Javier Hernandez (pichani) ambaye kwa sasa
anakipiga Bayer Leverkusen ya Ujerumani.
Pia, klabu
hiyo maarufu kama ‘Wagonga nyundo wa London’ inadaiwa wanawawinda Olivier
Giroud wa Arsenal na Michy Batshuayi wa Chelsea.
Wageni wenyeji wa Ligi
Kuu ya Uingereza, Newcastle United tayari wamekamilisha dili la kumsajili beki
kutoka Eibar ya Hispania, Florian Lejeune (26) kwa dau la pauni milioni 8.7 (sh
bilioni 23.49).
Kocha wa Newcastle
United, Rafael Benitez amesema kwamba; “Ni mchezaji ambaye amefanya vema nchini
Hispania. Nimemfahamu tangu akiwa Villarreal. Amekuwa akiimarika mara kwa mara.”
Lejeune amesaini dili
la miaka mitano katika klabu hiyo yenye makao makuu yake Tyneside.
The Sun linaripoti
kuwa ‘Washika Bunduki wa London’ Arsenal, wamepanga kutumia pauni milioni 70
(sh bilioni 154) kuwanasa ‘pacha’ wawili kutoka Ureno.
Pacha hao ni, William
Carvalho ambaye ni kiungo na mshambuliaji Gelson Martins kutoka katika klabu ya
Sporting Lisbon. Pia gazeti hilo limedai kuwa, Arsenal wako karibu kabisa
kumsajili mshambuliaji wa Olympic Lyon, Alexandre Lacazette.
No comments