Mtoto wa George Weah asaini mkataba wa miaka 3 na PSG

PARIS- TIMOTHY
Weah ambaye ni mtoto wa galacha wa mpira wa Liberia, George Weah, amesaini mkataba
wa kuitumikia klabu ya PSG kwa miaka mitatu.
Timothy ambaye
awali alikuwa kwenye timu ya watoto ya PSG, anafuata nyayo za baba yake ambaye aliwahi
kuitumikia klabu hiyo ya PSG kwa muda wa miaka 4 kuanzia mwaka 1992 hadi 1995.
Mshambuliaji
huyo wa miaka 17 ametia saini mkataba wa miaka 3 na PSG na kuhitimisha uvumi
ambao umekuwepo kwa muda mrefu kwamba, kinda huyo huenda akasainishwa mkataba rasmi
na timu hiyo.
Mnamo Septemba
2016, Timothy alifunga hat-trick katika ushindi wa bao 8-1 dhidi ya klabu ya
Ludogorets katika mechi yake ya kwanza ya Uefa.
“Ni fahari kubwa
kuendeleza pale baba alipoachia,” alisema Weah ambaye alizaliwa mjini New York
na kujiunga na New York Red Bulls kabla ya kujiunga na chuo cha mafunzo ya soka
cha PSG mnamo Julai 2014.
“Niko katika
klabu kubwa na natumai nitaendelea kuimarika ili niweze kuichezea timu kubwa,”
alisema Timothy.
BBC
No comments