Asubuhi Njema; Mourinho ataka fedha na Kroos kwa De Gea # Chelsea wamtaka Aguero # Wenger akata tamaa kwa Mbappe
LONDON- KOCHA wa Man United, Jose Mourinho amesema dili
lolote kutoka Real Madrid kwa kipa wake, David de Gea (26), lazima lihusishe
fedha na kiungo, Toni Kroos (27). Sun.
Baada ya kumsajili Tiemoue Bakayoko, Chelsea sasa imeelekeza nguvu zao
kwa mshambuliaji wa Man City, Sergio Aguero (29) ilia je azibe pengo la Diego
Costa ambaye ameambiwa anaweza kuondoka. Star.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amekata tamaa kuhusiana na mchakato wa
kumsajili mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe (18) na badala yake ameelekeza
nguvu zaidi kwenye usajili wa winga, Thomas Lemar (21) ambaye ameitaka Monaco
imuuze kwa Arsenal. Telegraph.
Borussia Dortmund wameongeza siku chache za kuendelea kusubiri ofa ya Chelsea
kwa mshambuliaji wao, Pierre-Emerick Aubameyang (28). Mail.
Chelsea imeeleza kuwa iko tayari kumpatia mkataba mnono wa miaka mitano,
winga wa Ubelgiji na Atletico Madrid, Yannick Carrasco (23). Express.
Tottenham Hotspurs wameongeza nguvu kwenye dili lao la kumsajili kiungo
wa Everton, Ross Barkley (23), licha ya ofa yao ya awali kukataliwa. Everton
pia wameripotiwa kudai kuwa, wako tayari kumuuza kiungo huyo. Independent.
Beki wa Southampton, Virgil van Dijk (26) anaweza kusajiliwa na
Liverpool, kwa dau la pauni milioni 60 (sh bilioni 174) na kuweka rekodi kwa
klabu hiyo ya Anfield baada ya kudaiwa kutakiwa na Arsenal kwa dau la pauni
milioni 45 (sh bilioni 130.5). Sun.
Arsene Wenger ameeleza kuwa, ana matumaini ya kumshawishi mshambuliaji
wake, Alexis Sanchez (28), ili aweze kubakia klabuni hapo Arsenal licha ya
kudaiwa kueleza kuwa anataka kuondoka. Mirror.
No comments