Header Ads

Simba kuanza mazoezi leo Chuo cha Polisi Kurasini



https://s.yimg.com/ny/api/res/1.2/30wxo5IiATHRY17rcgGDJg--/YXBwaWQ9aGlnaGxhbmRlcjtzbT0xO3c9ODAw/http://media.zenfs.com/en-GB/homerun/uk.goal.com/67ac716687ac2f008de12be77e437560
DAR ES SALAAM- TIMU ya soka ya Simba, inatarajiwa kuanza rasmi mazoezi ya kujifua kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi kilichopo Kurasini jijini hapa.

Hayo yanajiri siku chache, baada ya kuwasili kwa Kocha wa timu hiyo, Joseph Omog (pichani) kutoka kwao Cameroon alikokuwa kwenye mapumziko ya baada ya kuisha kwa ligi hiyo maarufu VPL.
Kocha huyo, anaamini amerejea nchini kwa kazi moja tu ya kuhakikisha anakisuka upya kikosi hicho ili msimu ujao kiweze kufanya vizuri katika michuano ya ligi kuu na ile ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Akizungumzia usajili wa timu hiyo, Omog amesema kuwa ni mzuri na wachezaji wote waliosajiliwa mpaka sasa anawajua, hivyo kazi kubwa aliyonayo ni kuwaunganisha ili waweze kucheza kitimu.
Chanzo; Bongo5

No comments

Powered by Blogger.