Header Ads

Upinzani wamtaka Mugabe ang’atuke madarakani



Chama cha Zanu-PF kimemteua bwana Mugabe kuwania urais mwaka ujao
HARARE- VYAMA vya upinzani nchini, vimemtaka Rais Robert Mugabe (93) ajiuzulu, na kumlaumu kwa kuiongoza nchi kutoka hospitalini kufuatia madai kuwa alisafiri kwenda Singapore kwa matibabu.

Kwa mujibu Msemaji wa chama kikuu cha upinzani cha MDC, Obart Gutu, vyama hivyo vinamtaka kiongozi huyo ajiuzulu kwani hawezi tena kwenda sanjari na mikiki mikiki ya uongozi.
Akizungumza na gazeti la binafsi la News Zimbabwe, Gutu alisema kwamba; “”Yeye si kijana tena kwani umri umeshamtupa mkono. Kuendelea kuwepo madarakani, ni sawa na kujiadhibu kwani hali yake si nzuri kimwili na kiakili.”
“Mugabe ni lazima aondoke na aiache Zimbabwe iweze kusonga mbele chini ya uongozi mpya.”
Kwa upande wake, Karauone Chihwayi, ambaye ni msemaji wa upande uliojitoa MDC alisema kwamba; “Nchi imekwama leo hii kwa sababu Rais wa Zanu anaongoza akiwa kitandani hospitalini.”
Chama cha Zanu-PF kimemteua Mugabe kuwania urais mwaka ujao, licha ya kuonekana kutokuwa na afya nzuri na amekuwa madarakani tangu mwaka 1980.
BBC

No comments

Powered by Blogger.