Ngeleja arudisha fedha za Escrow Serikalini
DAR ES SALAAM- MBUNGE wa Sengerema, William Ngeleja
amerejesha Serikalini (TRA) kiasi cha sh milioni 40.4 ambazo ni za mgawo wa Escrow
aliopewa na mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira.
Ngeleja
(pichani) alisema ingawa alipewa fedha hizo kama sehemu ya msaada, ameamua
kurudisha fedha hizo ili kukwepa kashfa hiyo ya ESCROW
“Fedha hizo
nilizipokea kwa nia njema kama msaada kutoka kwa ndugu yangu Rugemalira, ili
zinisaidie katika majukumu yangu ya kibunge na kutekeleza shughuli za kijamii
kama vile ujenzi wa makanisa, misikiti na kulipia karo za wanafunzi,”
“Vile vile,
nilipokea fedha hizo ili zinisaidie katika kutekeleza shughuli za kibunge
ambazo hazipo katika bajeti ya Serikali. Nilipokea Fedha hizo bila kujua kwamba
fedha hizo zilikuwa zinahusishwa na kashfa ya akaunti ya fedha za Escrow kama
ilivyo sasa,”
“Nilipokea
msaada huu kama wapokeavyo wabunge wengine, kwa nia njema. Nimepima na
kutafakari, na hatimaye nimeamua, kwa hiari yangu mwenyewe, kurejesha kiasi cha
Milioni 40.4 Serikalini (TRA),” alisema Ngeleja
Mbunge huyo
alipewa mgao huo wa fedha kiasi cha milioni 40.4 na Rugemalira kupitia Benki ya
Mkombozi mnamo Februari 12, 2014.
Chanzo; EATV
No comments