Sikumwambia baba lolote kuhusu mkutano na wakili – Trump Junior

WASHINGTON
DC- MTOTO wa kiume wa Rais Donald Trump, amesema kuwa hakumfahamisha baba yake
kuhusu mkutano na wakili raia wa Urusi ambaye alisema kuwa angesaidia katika
kampeni yake ya uchaguzi.
Donald Trump
junior alikiambia kituo cha habari cha Fox News kuwa, mkutano huo haukuhusu
chochote.
Katika hatua
nyingine, Trump Junior alitoa barua pepe zake zikionesha kuwa alikaribisha ombi
la kukutana na wakili, ambaye alikuwa na uhusiano na Urusi, mwenye ujumbe potofu
kuhusu Hillary Clinton.
Maofisa wa
Marekani wanachunguza madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani. Tangu
achaguliwe, Rais Trump ameandamwa na madai kuwa Urusi ilijumu kampeni ya Clinton.
Hata hivyo,
Trump amekuwa akikana kufahamu lolote na Urusi mara kwa mara imekana kungilia
kampeni hizo.
Alipoulizwa
ikiwa alimwambia baba yake kuhusu mkutano wa mwaka uliopita, Trump Junior
alisema hakukuwa na chochote cha kumwambia.
Donald Trump
Junior, mkwe wa Trump, Jared Kushner na mwenyekiti wa kampeni Paul Manafort,
walikutana na wakili wa Urusi, Natalia Veselnitskaya, katika jumba la Trump
Tower mjini New York mnamo Juni mwaka 2016.
BBC
No comments