Mchakato wa nani atachapa karatasi za uchaguzi hautuhusu Jubilee- Ruto
NAIROBI-
NAIBU Rais nchini, William Ruto amesema kwamba, chama cha Jubilee hakitashiriki
kwenye mikutano yoyote itakayoandaliwa na Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) ambayo
itahusiana na mustakabali wa kampuni gani ipewe zabuni ya kuchapisha karatasi
za kupigia kura.
Hayo
yanajiri siku chache, baada ya Mahakama ya Rufaa nchini kusitisha zabuni ya
uchapaji karatasi hizo ambayo awali ilitolewa kwa kampuni ya Al Ghurair ya
Dubai, na kuiagiza IEBC ibainishe kampuni nyingine itakayochapa karatasi hizo.
Akizungumza
jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Olenekenyu mjini Narok, Ruto alisema
suala la nani atachapa karatasi hilo haliwahusu Jubilee ila ziwepo tu hapo siku
ya uchaguzi huo Agosti 8 mwaka huu na kuongeza kuwa hawana ujuzi wala wataalam
wa kuchapa karatasi hizo.
“Hatuna
ujuzi huo wa kuchapa karatasi za kupigia kura. Tunaiachia IEBC mchakato mzima
wa kutafuta kampuni ya kuchapa. Kwetu sisi Jubilee, tutakuwa tukiwasubiri
wapinzani wetu hiyo Agosti 8, na kuwashinda warudi zao makwao,” alisema Ruto.
Aidha,
Ruto alitumia fursa hiyo kuwataka wapinzani waache kutoa vitisho kwa tume ya
uchaguzi vyenye nia ovu na kusema idadi ya kesi zilizofunguliwa na wapinzani dhidi
ya IEBC, zinalenga kuahirisha uchaguzi kwa kutumia mahakama.
“Sisi
Jubilee, tunataka kuwaambia NASA kuwa Wakenya wako tayari kupiga kura hiyo
Agosti 8, 2017 na wala si tarehe na siku nyingine. Wamekuwa wakifungua kesi
moja baada ya nyingine mahakamani, ili kuhujumu uchaguzi,” alisema Ruto.
Citizen Digital.
No comments