Sababu za Weston hotel kutofungwa zabainishwa
NAIROBI-
KUFUATIA wagonjwa 50 kulazwa kwa kuugua kipindupindu, imedaiwa kuwa chakula
walichokula kwenye hoteli ya kifahari ya Weston kilinunuliwa kutoka nje ya
hoteli hiyo.
Hoteli hiyo
inayohusishwa na umiliki wa Naibu Rais, William Ruto, imezua gumzo kwenye
mitandao kutokana na hatua ya Serikali kutoifunga licha ya kutoa wagonjwa 50.
Akizungumza kuhusu
sakata hilo, Waziri wa Afya nchini, Cleopha Mailu alisema uchunguzi uliofanywa
na wataalam wa wizara hiyo ulibaini kuwa hakukuwa na kirusi chochote cha
ugonjwa huo kilichokutwa kwenye jiko na wafanyakazi wa hoteli hiyo.
Wakati Weston
Hotel ikiwa haijafungwa, hoteli ya Jacaranda na mgahawa wa San Valencia ulifungwa
kutokana na wateja waliokula vyakula kulazwa kwa kuugua ugonjwa huo ambao
umeshaua watu wawili.
Inadaiwa hoteli
hizo zitafunguliwa pale tu wafanyakazi wake wote, watakapobainika kutokuwa na
virusi vinavyoeneza kipindupindu.
Standard Media.
No comments