Busu lakatisha maisha ya mtoto mchanga
Mtoto Mariana Sifrit akiwa kwenye mashine ya kumsaidia kupumua, muda
mfupi baada ya kufikishwa hospitalini. Mtoto huyo alifariki baadaye na inadaiwa
kuwa, aliambukizwa virusi hatari vya HSV-1 kupitia busu.
IOWA- IMEKUWA ni habari ya kusikitisha na kuogofya, baada
ya mtoto mwenye umri wa siku 18 kuugua ghafla na kufariki dunia kutokana na
kuambukizwa ugonjwa kupitia busu.
Kwa mujibu
wa Idara ya Afya ya New York, Mariana Sifrit aliugua ugonjwa ambao ulisababisha
mauti yake baada ya kuambukizwa virusi vya HSV-1 ambavyo ni hatari zaidi kwa
watoto kwani wanakuwa hawana kinga kama walivyo watu wazima.
Mariana aliyezaliwa
Julai mosi mwaka huu, anadaiwa kupigwa busu mmdomoni na mtu ambaye
amemuambukiza ugonjwa huo na wazazi bado hawajajua ni nani aliyetekeleza tukio
hilo kwani wao walipochunguzwa kama wana virusi hivyo walionekana kuwa hawana.
Inadaiwa kuwa
virusi hivyo vya HSV-1, huambukizwa kwa mtoto kutoka kwa mtu mzima mwenye midomo
yenye ubaridi mkali.
Akizungumza kuhusu
mkasa uliomkumba mwanae, Nicole Sifrit alisema aliruhisiwa kutoka hospitalini
na mwanawe akiwa na nyaraka zinazoonesha kuwa yupo salama lakini baada ya siku
sita kupita, hali ilibadilika na mtoto kurudishwa hospitalini akiwa hoi
taabani.
Alikuwa akisumbuliwa
na Ini ambalo lilishindwa kufanya kazi vema, huku damu ikivuja ndani kwa ndani
na kushindwa kuganda. Madaktari walibaini kuwa, mtoto huyo aliambukizwa virusi
vya HSV-1, ambavyo huambukizwa kwa busu.
“Watu wazima
wengi wameathiriwa na na virusi vya HSV-1, na huwa wana virusi hivyo kwenye
midomo na mate yao kwa muda lakini hawaoneshi dalili,”
“HSV-1
huenea pale mate ya mtu aliyeathiriwa na virusi hivyo vinapogusa tundu za pua
au kuingia kwenye ngozi. Wakati virusi hivyo kwa watu wazima husababisha midomo
kuwa ya baridi sana, lakini kwa watoto wachanga huwa hatari zaidi kwani
husababisha vifo,” ilieleza taarifa ya Idara ya Afya na Usafi wa Akili ya jiji
la New York nchini hapa.
Mara baada
ya kufariki dunia kwa mwanaye, mzazi wa Mariana aliandika kwenye ukurasa wake
wa Facebook kwamba; “Kila mzazi anapaswa amlinde mwanaye, kwa kutoruhusu mtu
yeyote ambusu.” Ikiwa ni ushauri wake kwa marafiki wake mtandaoni humo..
CBS NEWS
No comments