Header Ads

Rooney asema anaisubiri kwa hamu ziara ya Tanzania



Wayne Rooney is back with his boyhood club
LIVERPOOL- NYOTA wa soka wa Uingereza, Wayne Rooney, ambaye amekamilisha uhamisho wake kutoka Manchester United na kurejea Everton, amesema anasubiri kwa hamu kubwa kuzuru Tanzania.

“Naisubiri sana kwa hamu na ghamu (safari ya kwenda Tanzania) - naamini kuwa itakuwa safari nzuri. Itakuwa nzuri sana na natumai kwamba nitaweza kuingia uwanjani na kucheza.
“Huwa vizuri sana unaposafiri na timu. Ni vizuri kuwa hotelini na wachezaji, kujumuika nao na kuwafahamu zaidi. Sijawahi kwenda Tanzania, hivyo nasubiri sana kwenda huko,” alisema Rooney.
Rooney atakuwa kwenye kikosi cha Everton kitakachocheza mechi ya kujiandaa kwa msimu ujao Tanzania. Amesema ziara hiyo, itampa fursa mwafaka ya kufahamiana na wachezaji wenzake wapya.
Rooney anayeongoza kwa ufungaji mabao Uingereza, alitia saini mkataba wa miaka miwili Goodison Park Jumapili.  Rooney alifika mazoezini USM Finch Farm leo Jumatatu na anapangiwa kuungana na wenzake kwa safari hiyo ya Tanzania baadaye wiki hii.

No comments

Powered by Blogger.