Rais wa Zambia atangaza hali ya dharura

LUSAKA- RAIS
Edgar Lungu ametangaza hali ya dharura nchini, kutokana na moto mkubwa ulioteketeza
soko kuu mjini hapa.
Moto huo
pamoja na visa vingine kama hivyo, unadhaniwa kuanzishwa kwa maksudi na Rais
Lungu (pichani) anasema ni vitendo vya kuhujumu uchumi ili kuifanya Zambia isitawalike
vyema.
Hata hivyo,
wapinzani wake wanasema Rais Lungu anatumia mikasa hiyo kama kisingizio cha
kuendeleza utawala wa kiimla.
No comments