Marekani yadai itatumia nguvu za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini iwapo italazimika

WASHINGTON DC- MAREKANI imesema kuwa itatumia nguvu za kijeshi
dhidi ya Korea Kaskazini, ‘iwapo ni lazima’ kufuatia jaribio la kombora la
masafa marefu lilotekelezwa na taifa hilo.
Balozi wa
Marekani, Nikki Haley (pichani) alisema kuwa maamuzi mapya pia yatawasilishwa dhidi ya Korea
Kaskazini katika Umoja wa Mataifa (UN).
Alielezea
jaribio hilo kama tishio la kijeshi mbali na kutishia kutumia vikwazo vya
kibiashara. Jaribio hilo la kombora la hivi karibuni, ni miongoni mwa majaribio
mengine yanayokiuka marufuku ya UN.
Wakati
huohuo, Waziri wa Ulinzi nchin,i James Mattis na mwenzake wa Japan, Tomomi
Inada, walisema kuwa jaribio hilo ni uchokozi ambao hautakubalika.
Taarifa iliyotolewa
na Wizara ya Ulinzi imesema kuwa, wawili hao walizungumza kwa njia ya simu
ambapo Jenerali Mattis alisema Marekani itaendelea kuilinda Japan.
Haley alisema
jana kwamba, jaribio la kombora la masafa marefu la Korea Kaskazini (ICBM)
linaangamiza suluhu ya uwezekano wa mazungumzo ya kidiplomasia
“Marekani
imejiandaa kutumia uwezo wake wote kujilinda na washirika wetu,” Haley aliliambia
baraza la usalama katika Umoja wa Mataifa, ambalo lilikutana kwa kikao cha
dharura kuzungumzia hatua hiyo ya Korea Kaskazini.
“Moja ya
uwezo wetu upo katika jeshi. Tutautumia iwapo tutalazimika kufanya hivyo, lakini
tungependelea kutoelekea upande huo,” alisema.
Haley ambaye
alieleza kuwa alijadiliana na Rais Donald Trump, alisema kuwa Marekani pia
inaweza kukata biashara na mataifa ambayo yanaendelea kufanya biashara na Korea
Kaskazini kwa kukiuka maamuzi ya UN.
“Tutayaangazia
mataifa ambayo yanaendelea kufanya bishara na utawala huu usiofuata sheria,” alisema.
BBC
No comments