Ajali ya lori la mizigo yaua watu 80 CAR

BANGUI-
AJALI ya lori moja la mizigo nchini Jamhuri ya Afrika ya kati (CAR),
imesababisha vifo vya zaidi ya watu 80, wengi wakiwa wachuuzi waliokuwa
wakielekea sokoni katika mji wa Bambari.
Walioshuhudia
tukio hilo, wamesema lori hilo lilikuwa limebeba watu wengi na kujazwa mizigo
kupindukia, huku likiendeshwa kwa mwendo wa kasi wakati lilipopinduka.
Maofisa wa usalama
barabarani wamelaumiwa kwa kutochukua hatua kuzuia ukiukwaji huo wa sheria za
barabarani.
BBC
No comments