Rais Bouteflika aitaka Ufaransa iiombe radhi Algeria
ALGIERS- RAIS
Abdelaziz Bouteflika kwa mara nyingine ameitaka mkoloni Ufaransa iiombe radhi
rasmi Algeria, kutokana na jinai kubwa ilizowafanyia wananchi wa Algeria wakati
wa utawala wa kikoloni.
Bouteflika
alisema hayo jana, wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru na kusisitiza
kuwa, Waalgeria wanaitaka Ufaransa iwaombe radhi kutokana na ukatili, mateso na
masahibu yaliyosababishwa na taifa hilo wakati wa utawala wake wa kikoloni kwa
miaka 132.
Hayo
yanajiri katika kipindi ambacho Ufaransa ina Rais mpya, Emmanuel Macron, ambaye
awali kabla ya kushinda kiti hicho alishawahi kuitembelea Algeria na kukiri
kuwa ukoloni uliliathiri kwa kiasi kikubwa taifa hili.
Macron ambaye
aliitembelea Algeria mnamo Februari mwaka huu, wakati alipokuwa anagombea urais
wa Ufaransa, alikiri ukoloni wa nchi yake uliofanyika katika miaka ya kuanzia
1830 hadi 1962 ilikuwa ni jinai dhidi ya binadamu.
Zaidi ya
watu milioni moja nchini, waliuliwa na wakoloni katika vita vya ukombozi.
Pars Today
No comments