Header Ads

Mwanamuziki mkongwe afariki Dar es Salaam



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiGpWtO1b2ubUP387apJtQx7CMXju6E612vpEhH1Vw22Qrv-YCf8E8tZNpoEVf6POeIibowVUjUVZc3kvkOBikNhR8eoQaGuKYWFlugvjyQcSwDIM_3snKQbRCG5EsufMxaZgXt8XF64Kr2/s1600/IMG_8199.jpg
Mwanamuziki mkongwe nchini, Shaaban Dede amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu, kwa takriban wiki mbili.

Habari zilizothibitishwa na mtoto wa nguli huyo, Hamad Dede, zimeeleza kuwa baba yake alifariki leo saa mbili asubuhi hospitalini hapo.
Hamad alisema mipango ya maziko inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala, na ratiba na taratibu zote zitatangazwa mara zitapokamilika kupangwa.

Marehemu Dede atakumbukwa kama mmoja wa wanamuziki nguli kutokea nchini Tanzania, kwa sauti yake tamu na utunzi wa nyimbo mbalimbali zilizoshika chati akiwa na bendi mbalimbali zikiwemo Tabora Jazz, Bima Lee, Mlimani Park na Mondo Ngoma ambako alikuwa anatumikia hadi maiti yamemkuta.
Jamii Forum

No comments

Powered by Blogger.