Pacquiao ataka video ya pambano lake na Horn ipitiwe upya

MANILA- MKALI wa ngumi nchini, Manny Pacquiao ameunga
mkono hoja zinazoenea mitandaoni za kutaka kufanyike kwa mapitio ya video ya
pambano la ngumi baina yake na Muasutralia, Jeff Horn.
Pambano hilo
lililopigwa Jumapili iliyopita, liliibua utata kutokana na Horn kupewa ushindi
na majaji wote watatu licha ya kuonekana kupigwa ngumi nyingi zaidi.

Jeff Horn
Akitoa taarifa
yake kama Seneta, Pacquiao amesema anaunga mkono mwito wa chama cha ngumi
nchini (GAB), ambacho kinataka kufanyika kwa mapitio ya video hiyo ili kubaini
nani mshindi halisi.
“WBO
inatakiwa ichukue hatua stahiki kuhusiana na barua iliyotumwa kwao na GAB, ili
kuepusha kumomonyoa maadili ya mchezo na matakwa ya wapenda mchezo huo”
ilieleza taarifa ya Pacquiao.
Aidha,
taarifa hiyo ilieleza kuwa bondia huyo alikubali maamuzi hayo lakini akiwa
kiongozi na mpiganaji ngumi, hana budi kudumisha na kupambana kwa ajili ya
upatikanaji wa haki, uwazi na usawa kwa ajili ya umma.
“Ninaupenda
mchezo wa ngumi na sipendi kuuona ukifa, kwa sababu ya maamuzi mabovu kutoka
kwa maofisa wake,” ilieleza taarifa hiyo.
CNN
No comments