R Kelly adaiwa kuwanyanyasa wanawake kingono
Wakili
wa mwanamuziki huyo, alisema kuwa atatumia kila njia kuhakikisha kuwa wale
wanaomtuhumu anawakabili kisheria ili kusafisha jina lake.
Ripoti
ya BuzzFeed, imemtuhumu mwanamuziki huyo kwa kuwabadili kimawazo wanawake walio
karibu naye kwa lengo la kuimarisha usanii wao wa muziki.
Kelly
amewahi kukabiliwa na tuhuma za dhulma za kingono, lakini hakupatikana na
hatia. Amekana kufanya makosa yoyote.
Ripoti
hiyo iliowanukuu wazazi watatu, inasema kuwa hawajawasiliana na watoto wao kwa
miezi kadhaa, na kwamba wanawake hao wote wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 18
walikuwa wakidhibitiwa na msanii huyo.
Udhibiti
huo unashirikisha chakula wanachokula na nguo wanazovaa, wakati gani wa kuoga
na kulala mbali na kufanya tendo la ngono, yote hayo yakirekodiwa na msanii
huyo.
Wanachama
watatu walio karibu na mwanamuziki huyo, pia walihojiwa na kusema kuwa wanawake
sita wanaishi katika nyumba zinazosimamiwa na msanii huyo.
Iwapo
watavunja sheria, wanasema wanawake hao huadhibiwa kwa kupigwa mbali na
kutukanwa na msanii huyo kulingana na ripoti hiyo.
Baadhi
ya wazazi wao wameripoti wasiwasi wao kwa polisi, lakini wanawake hao wanasema
kuwa wamekubali kuishi katika nyumba hizo.
Wakili
wa msanii huyo, Linda Mesch alisema; “Robert Kelly ameshangazwa na kukerwa
kuhusu madai hayo mapya anayodai kutekeleza.”
BBC
No comments