Mwanamke aliyevaa nguo fupi kuchunguzwa Saudia
Mwanamke
huyo ambaye ni mwanamitindo aitwaye Khulood, alisambaza video hiyo akitembea
katika ngome ya kihistoria ya Ushayqir.
Kanda
hiyo ilizua hisia na mjadala mkali, huku wengine wakitaka akamatwe kwa kuvunja
sheria kali ya uvaaji wa mavazi nchini. Raia wengine walimtetea mwanamke huyo
wakimsifu kwa ujasiri wake.
Wanawake
nchini ni sharti wavae nguo zisizowabana na ndefu, zajulikanazo kama ‘abaya’
hadharani pamoja na kitambaa kichwani. Pia, hawaruhusiwi kuendesha magari na
hutengwa na wanaume wasio kuwa na uhusiano wa kifamilia.
Katika
video hiyo iliosambazwa katika mtandao wa Snapchat wikendi iliyopita, Khulood anaonekana
akitembea katika barabara isiyo na watu katika ngome hiyo ya historia ya
Ushayqir yapata kilometa 155, Kaskazini mwa mji huu wa Riyadh mkoani Najd.
Najd
ni miongoni mwa maeneo ya kihafidhina nchini. Ni eneo ambalo mwanzilishi wa
Wahabi alizaliwa katika karne ya 18.
Video
hiyo ilichukuliwa na watumiaji wa mtandao wa Twitter nchini, ambapo kulikuwa na
mjadala mkali kati ya wale wanaoamini Khulood angepaswa kuadhibiwa na wengine
waliosisitiza kuwa anafaa kuachwa kuvaa anachotaka.
BBC
No comments