Header Ads

Ujumbe wa mtandaoni wavunja ndoa Taiwan



https://ichef-1.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/1805E/production/_90289389_reutersline033233438.jpg

TAIPEI- Umewahi kupuuza ujumbe wa mpenzi au mchumba wake kwenye mitandao ya kijamii? Basi unapaswa uelewe kwamba ujumbe huo unaweza ukatumika kama ushahidi ambao utasababisha uhusiano au ndoa yenu ivunjwe na mahakama.
Mwanamke mmoja nchini, ameruhusiwa kumpa talaka mume wake, kwa kutumia ishara kwamba ujumbe wake aliomtumia mumewe ulisomwa kama ushahidi kwamba mumewe alimpuuza.
Mtandao wa kijamii wa Line unaonesha mumewe alikuwa akifungua ujumbe huo, lakini hakujibu. Ushahidi huo, umesababisha Jaji ambaye alikuwa akisikiliza shauri hilo amkubalie mwanamke huyo ombi la kumtaliki mumewe.
Mwanamke huyo alitumia alama za rangi ya bluu, ambazo hutumiwa na mitandao kama vile Line na WhatsApp mtu anaposoma ujumbe, kudai kwamba mumewe alikuwa ameupokea ujumbe.
Jaji Kao wa mahakama ya masuala ya kifamilia, Hsinchu, amesema hali kwamba mwanamume huyo alipuuza ujumbe huo, ni ushahidi kwamba ndoa kati ya wawili hao haiwezi ‘kuokolewa’ na vyombo na kuwaruhusu kupeana talaka.
https://ichef-1.bbci.co.uk/news/624/media/images/78799000/jpg/_78799271_whatspp2.jpg
Katika kipindi cha miezi sita hivi, mwanamke huyo ambaye jina lake la ukoo ni Lin, alimtumia mumewe ujumbe mara kadhaa, wakati mmoja ikiwa ni baada ya kulazwa hospitalini baada ya kupata ajali barabarani.
Katika ujumbe mmoja, alimwambia mumewe kwamba alikuwa katika chumba cha dharura hospitalini na akamuuliza ni kwa nini anasoma ujumbe wake lakini hamjibu.
Ingawa mumewe alimtembelea hospitalini mara moja, mahakama ilisema kwamba kitendo cha kupuuza ujumbe huo ni msingi tosha wa kumpa talaka.
“Mshtakiwa hakumjulia hali mlalamishi, na habari aliyotumiwa na mlalamishi aliisoma lakini hakujibu,” mahakama ilisema kwenye uamuzi wake.
Ilikuwa ni baada ya mwezi mmoja au miwili hivi, baada ya ajali hiyo, ndipo mumewe alimtumia ujumbe mfupi.
“Ujumbe wake ulikuwa unamhusu mbwa wao, na alimfahamisha pia kwamba kulikuwa na barua iliyotumwa kwake, lakini hakuonesha ishara za kutaka kujua hali yake,” Jaji Kao alisema.
Wawili hao walifunga ndoa 2012. Mwanamke huyo ambaye amewahi kuolewa awali ana miaka 50 hivi na mumewe ana miaka 40 hivi.
BBC


No comments

Powered by Blogger.