Putin na Jinping wapinga ufungwaji wa mtambo wa THAAD Korea Kusini
MOSCOW- RAIS Vladimir Putin na mgeni wake, Xi Jinping wa
China, wamepinga ufungaji wa mitambo ya kutungua makombora wa Marekani (THAAD) ambao
umefanyika nchini Korea Kusini.
Aidha, kwa viongozi
hao kwa pamoja wamekubaliana kuendeleza uhusiano baina ya China na Urusi baada
ya kukutana mjini hapa sanjari na kuongeza juhudi zao kutatua mgogoro wa Korea
Kaskazini.
Hayo
yalijiri jana baada ya viongozi hao kukutana katika Ikulu ya Kremlin mjini
hapa, mara baada ya kuwasili kwa kiongozi huyo wa China na kufanya mazungumzo
rasmi ikulu.
Kwa muda
mrefu, China imekuwa ikidai kuwa mitambo hiyo ya THAAD ambayo imekuwa ikifungwa
Korea Kusini, inachochea vurugu kwenye rasi hiyo ya Korea na pia inaipeleleza
China.
CNTV
No comments