Header Ads

Pakistan yaanza mashambulizi dhidi ya Islamic State



wanajeshi wakilinda usalama
ISLAMABAD- WANAJESHI wa Pakistan, wameanzisha operesheni kubwa ya kijeshi dhidi ya wapiganaji wa Islamic State (IS) katika mkoa wa Kaskazini Magharibi, ulio karibu na mpaka wa Afghanistan.

Msemaji wa Jeshi nchini, amesema kwamba wapiganaji hao wenye itikadi kali wamejiimarisha ndani ya Afghanistan na hivyo wanapaswa kuzuiwa kufanya hivyo ndani ya Pakistan.
Operesheni hiyo inalenga zaidi kufanywa katika mkoa wa mpakani, huku ikiungwa mkono na jeshi la Anga la Pakistan.
Serikali imekuwa ikikanusha uwepo wa kundi hilo la IS ndani ya nchi, licha ya mfululizo wa mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na kundi hilo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

No comments

Powered by Blogger.