Header Ads

Korea Kusini yataka mazungumzo ya kijeshi na Korea Kaskazini



South Korean solders at a border village
BERLIN- KOREA Kusini imependekeza kufanyika kwa mazungumzo ya kijeshi na Korea Kaskazini, baada ya majuma kadhaa ya msukosuko, inayotokana na taifa hilo kufanya majaribio ya mara kwa mara ya makombora yake.

Ikiwa mazungumzo hayo yatafanyika, yatakuwa ndiyo ya kwanza ya juu kufanyika tangu mwaka 2015.
Maofisa wa vyeo vya juu Korea Kusini, wamesema kuwa mazungumzo hayo yatalenga kisitisha vitendo vyote ambavyo huchangia kuwepo kwa misikusuko ya kijeshi katika eneo lenye ulinzi mkali kati ya Kusini na Kaskazini.
Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in tangu mwanzo alikuwa ameashiria kuchukua hatua ya kuleta ushirikiano wa karibu na Korea Kaskazini.
Akihutubia hivi karibuni mjini hapa, Jae-in alisema mazungumzo na Korea Kaskazini yanastahili kufanyika na kutaka mwafaka kuafikiwa.
Lakini, hatua za Korea Kaskazini kuyafanyia majaribio makombora likiwemo la hivi karibuni la masafa marefu, yanaenda kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa.
Naibu Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini, Suh Choo-suk, aliwaambia wanahabari kuwa, mazungumzo yatafanyika eneo la Tongilgak, katika jengo la Korea Kaskazini katika eneo lisilo na ulinzi mkali kati ya nchi hizo mbili.
BBC

No comments

Powered by Blogger.