Pacquiao amepigwa kihalali- majaji
BRISBANE- MATOKEO ya pambano la ngumi kati bondia maarufu duniani na
mwanasiasa wa Ufilipino, Manny Pacquiao, na mwalimu Jeff Horn wa Australia
yamebaki kama yalivyokuwa hapo awali.
Uamuzi huo umetoka baada ya majaji watano kutoka sehemu mbalimbali
duniani, ambao waliitwa na Chama cha Ngumi cha WBO kutoa maamuzi hayo ambayo ni
pigo kwa Pacquiao ambaye alidai kuwa mpinzani wake alipendelewa.
Mara baada ya Pacquiao kuomba mapitio hayo, WBO iliitisha majaji hao
ambao walikaa kwa muda ambao haujawekwa wazi ili kupitia video hiyo bila sauti
na kubaini kuwa Pacquiao alishinda raundi tano wakati Horn alishinda raundi
saba.
Kwa matokeo hayo, ushindi wa Horn ambao awali ulisitishwa hadi maamuzi
ya majaji hao yatoke, umerudishwa kama ilivyokuwa awali.
Aidha, WBO ilisisitiza kuwa uchunguzi huo ulifanyika kwa minajili ya
kuongeza uwazi kwenye michezo hiyo na kukomesha dalili zozote za ulaghai na
uonevu.
BBC Sport.
No comments